Makanisa ya Kikristo ya Mungu
[066]
Mipagilio ya Sikukuu
(Toleo1.0 20040306-20040306)
Jarida hili limetungwa kwa lengo la kuwasaidia Waandaaji wa Sikukuu katika mipango yao ya uandaaji wa Sikukuu. Inatarajiwa kwamba majukumu mengi yatakabidhiwa kwa wasaidizi wengine. Pia inatilia maanani kuzingatia kuwa watu wengi watakaohudhuria Sikukuu kwa mara ya kwanza hawatafahamu wanachotarajiwa kufanya au kinachohitajika katika mpango mzima wa maandalizi ya Sikukuu. Wakati mwingine utahitajika sana moyo wa utayari ili kuendana sambamba kuhusiana na mahitaji ya watu wa makundi mengine na mataiafa wakati wa kuandaa kambi la Sikukuu.
Christian Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Copyright © 2004 Christian Churches of God, Ed. Wade Cox)
Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org and http://www.ccg.org
Mpangilio wa Sikukuu
Utangulizi
Maufanikio ya kambi ya Sikukuu yanategemea na umakini wa timu ya waandaaji, wanenaji, wasaidizi, na mwitikio wa kila mmoja binafasi waliohitajika kufanya kitu Fulani, au waliojitolea, kuchukua majukumu katika eneo lolote la maongozi ya Sikukuu, ka namana yoyote ile iwe kwa sehemu ndogo au kubwa. Tupo pale kwa kufanya mambo yote mawili yaani kutumikiwa na kuwatumikia wengine kwa upendo na ushirikiano.
Mara tatu kwa kila mwaka Watu wa Mungu wameamriwa kuyaacha maskani yao na kwenda katika mahali alipopachagua Mungu aliweke Jina lake (Kut. 23:14-17; Law. 23:1-44; Kum. 16:1-6). Tunaenda katika kambi za Sikukuu ili kwenda kujifunza jinsi ya kumuabudu na kumcha Mungu (Kum. 4:10; 10:12-13; 14:23; 17:19; 31:12). Tunatakiwa twende na watumishi wetu wa kiume na wakike wanaokaa pamoja nasi malangoni mwetu ili nao wajifunze jinsi ya kumushia Mungu kikamilifu (Kum.12:7,12; 14:29; 16:11-14).
Je, ni kina nani hawa watumwa wa kiume na wakike kwa leo? Watu wengi siku za leo hawana watumwa, hivyo basi ni kina nani basi tunaowaongelea hapa? Kimsingi, ni wale ambao tunawaajiri majumbani mwetu ili watusaidie kazi. Hii ndio sababu mojawapo inayotufanya tusiende kwenye mahoteli kununua chakula siku za Sabato, kwa sababu kwa njinsi wanavyotutumikia siku zile wanafanyika sawasawa kabisa kama watumwa walivyotumikia mabwana zao. Na wale wengine tuliowaajiri kwenye miradi yetu mingine, kama wameamini, wapewe ruhusa kazini ili wajiunge na sisi kwenye Sikukuu. Hatahivyo, hatupaswi kuwaomba watu watutumikie wakati wowote ule ambao Mungu anawatazamia watajihudhurisha kwake na kumuabudu. Ujinga au uasi wao usitufanye sisi tuchukulie kama ni kitu cha faida kwetu kwa kuwafanya watutumikie kwa wakati huo.
Katika Makanisa ya kikristo ya Mungu tunatumia Kalenda ya Mungu kama watu wa Mungu walivyokuwa wanaitunza kwa zama mbalimbali za miaka ya nyuma. Kwa maelezo zaidi angalia jarida lisemalo Kalenda ya Mungu [156] na majarida yanayo endananayo.
Kabla ya kuanza kwa Sikukuu yoyote wanaume wantatakiwa watumie masaa kadhaa kwa kuandaa mahubiri na mambo ya kushirikisha kwa mwongozo wa neno katika yale yaliyoulizwa majumbani.(1Ko. 14:34-35; 1Tim. 2:8-15). Wanawake wanayo majukumu kadhaa mbalimbali mengine na kazi mbalimbali, kama vile kulea watoto na kuwaeleka, kuwatembelea na kuwapelekea neno wagonjwa na kuwafariji waliokata tama, kadhalika na kuhudhuria vipindi vya mafundisho ya Biblia na majadiliano yake. Ili kupata maelezo zaidi kuhusu majukumu na kazi za akina mama soma jarida lisemalo Majukumu ya Mama Mkristo [062]. Ni hakika kabisa kuwa majukumu ya kina mama wakati wa Sikukuu hizi ni kuhakikisha washiriki wanajisikia wamehudhuria Sikukuu yenye furaha.
Jinsi ya Kuandaa kambi la Sikukuu
Waandaaji wa kambi la Sikukuu wanapaswa kuandaa vizuri mahali pa kambi mapema iwezekanavyo kwa kuzingatia panakuwa salama, patulivu, malzi safi, ikitegemea na hali ya kiuchumi ya kifedha ya wahudhuriaji. Ukumbi wa mkutano na jiko zinatakiwa zive na ukubwa unaoshabihiana na view na vifaa vyote vinavyohitajika kuwahudumia washiriki kwa wakati mmoja. Tangazo la mahali itakapowekwa kambi na gharama zinazotarajiwa kulipwa na kila muhudhuriaji inapaswa vitolewe mapema iwezekanavyo na kwa ufasaha sana kabla ya siku ya Sikukuu haijafika. Na kama inawezekana, mwandaaji na/au mwakilishi wake wawe wamezoeleka na kufahamika katika eneo lile. Hii pengine itakuwa na maana ya kuafamu pia ilipo zahanati ya eneo lile na zilipo huduma nyingine muhimu na mahali penyekuvutia watu kwa kufanya shughuli nyinezo, nk.
Mwaandaaji ahakikishe kuwa wanenaji wamejiandaa vya kutosha na masomo ya kujadiliwa yameshawekwa katika hali nzuri isiyoweza kuwachanganya watu.
Wahudhuriaji lazima wathibitishe nia yao ya kuhudhuria mapema, na kukiwepo mabadiliko yoyote yahusuyo Sikukuu basi aharifiwe muandaaji mapema sana. Kama kunamtu ambaye atatakiwa apokelewe uwanja wa ndege, nk, wanaweza kuomba msaada huo ila watoe taarifa mapema iwezekanavyo ili kwamba usafiri uandale mapema kuwachukua uwanja wa ndege. Iwapo mpangilio wa usafiri unaonekana kusababisha uchelewaji katika kuja kuchukuliwa uwanjani, basi, utaangaliwa uwezekano mwingine ikilazimu wa kungojelea hadi ndege itakayofuata ili kuchukuliwa kwa pamoja na mgeni mwingine. Muda muafaka unatakiwa uruhusiwe ili kumhakikishia kila mmoja awe kambini kwa wakati ili aweze kujiandaa vizuri kwa ajili ya ibada ya kwanza. Tunapaswa kujua kuwa kama tutakuwa tunachelewa chelewa, ndipo tutamlazimisha mwingine achelewe pia. Ni wajibu wa kila mtu kuhakikisha kuwa muda muafaka unatakiwa kwa kufanya safari.
Yeyote anayehitaji msaada wa kifedha atatkiwa kulijadili hili na mwangalizi wa eneo lakeo.
Yeyote mwenye matatizo ya ulaji wa aina fulani ya vyakula atoe taarifa kwa mwandaaji wa Sikukuu ili kwamba awataarifu wahusika wanaoshughulikia uandaaji wa mambo mbalimbali.
Ukumbi wa Mkutano
Iana yoyote ya mapambo ya kipagani au sanamu lazima ziondoshwe katyika ukumbi huu wa mkutano. (pia katika vyumba vya kulala).
Jozi ya vipaza sauti vinatakiwa vikaguliwe na kujaribiwa, bila kusahau chumba cha wamama.
Sakafu na lisafishwe kwa deki au ufagio na viti na meza viandaliwe katika mpangilio mzuri.
Matangazo yafanyike kila siku ili kuwahakikishia watu kuwa wanaifahamu ratiba ya siku ile na washughulike na jambo lolote litakalokuwepo.
Mpango wa dharura kama wa zimamoto na mahali pa kupata msaada wa Huduma ya Kwanza, inatakiwa vielezwe na ikiwezekana, utaratibu wa mahali zilipo waweza kubandikwa kwenye ubao wa matangazo.
Ratiba ibandikwe kwenye ubao wa matangazo na nakala nyingine zigawanywe kwa kila mhudhuriaji. Ratiba hizi zijumlishe maekezo ya siku na muda wa ibada na/au masomo ya Biblia, shughuli za kimakundi na maeneo ya kupata chakula na muda wa kula chakula.
Chumba cha Wamama
Ikiwezekana, kiwepo chumba maalumu kwa ajili ya kushughulikia mahitaji mbalimbali ya wamama kama vile sehemu ya kulishia chakula watoto wachanga au kuwanyonyesha na kuhudumia watoto wadogo. Kinaweza pia kutumika kama darasa la Biblia la watoto na kuwaepusha na hali yao ya utundu au upigaji makelele ya minong’onezano. Vipaza sauti vitoe sauti yenye kuhakikisha kuwa wamama wanapokuwa kwenye chumba hiki wakiwahudumia watoto wasikose kusikia ujumbe unaoendelea kufundishwa.
Ibada
Waandaaji wa wahudumu wanapaswa watakuwa na wajiku wa jumla kuhakikisha kuwa ukumbi umeandaliwa na masuala yote yahusuyo ibada yameandaliwa sawasawa na yako tayari.
Ukumbi unatakiwa uandliwe muda kabla na liwe safi na maridadi. Kabrasha zote zinazohusiana na ibada ile zigawiwe kwa watu mapema.
Jozi la vipaaza sauti vikaguliwe na vijaribiwe.
Nyimbo husika, vitabu vya nyimbo, na muziki lazima viandaliwe na view tayari.
Matangazo yoyote apewe kiongozi wa uimbaji, au mtu mwenye majukumu sawa na yeye kisha yabandikwe kwenye ubao wa matangazo kwa ajili ya watakaokosa kupata.
Wimbo maalumu waweza kuandaliwa na kuwekwa kwenye ratiba katika hali muafaka.
Ibada zianzie kwa kufuata muda sahihi uliopangwa na maandalizi yote yawe yamekamilka.
Mhudumu wa mambo ya chakula ahakikishe kuwa maji yameandaliwa kwa ajili ya wanenaji na kuwa mengine yamewekwa nyuma ya ukumbi kwa ajili ya yeyote atakaye yahitaji.
Huduma ya chakula katika Sikukuu
Kwanini tunakula pamoja
Makanisa ya Kikristo ya Mungu tunaamini umuhimu wa kula pamoja. Wapenwa wengi wa Makanisa ya Mungu wanatarajiwa kula chakula cha pamoja katika Usiku wa Kuangaliwa. Katika Kumbukumbu la Torati 16:17 tumeambiwa kupika na kula katika mahali alipopachagua Mungu. Wakati huu wa Usiku wa Kuangaliwa watoto wadogo watauliza “Je, nini maana ya jambo hili?” Tena, wengi wao hawapo nje ya makazi yao, na kusaidiwa kupikiwa chakula mahali alipopachagua Mungu. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuutunza kikamilifu Usiku wa Kuangaliwa, angalia jarida lisemalo Jinsi ya kuandaa Mlo wa Pasaka katika Usiku wa Kuangaliwa [093]. Katika fungu lifuatalo la maandiko kutoka Kumbukumbu la Torati tutasoma jinsi Mungu alivyotuamuru katika kila Sikukuu kama hivi:
Kumbukumbu la Torati 14:23,26 23Nawe utakula mbele za BWANA, Mungu wako, mahali atakapopachagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng’ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha BWANA, Mungu wako, daima. 26na zile fedha zitumie kwa chochote itakachotamani roho yako, ng’ombe, au kondoo au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako chochote; nawe utakula huko mbele za BWANA, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako;
Kumbukumbu la Torati 16:11,14 11nawe utafurahi mbele ya BWANA, Mungu wako, wewe na mwana wako na binti yako, na mtumwa wako na mjakazi wako, na mlawi aliye ndani ya malango yako, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio katikati yako, katika mahali atakapo chagua BWANA, Mungu wako, apakalishe jina lake. 14nawe utafurahi katika idi yako, wewe, na mwanao, na binti yako, na mtumwa wako, na mjakazi wako, na mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako.
Pia tazama Kumbukumbu la Torati 12:6-8 na 17-18
Kumbukumbu la Torati 12:6-8 6 elekeni huko sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu, na sadaka zenu za hiari, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ng’ombe nay a kondoo; 7 a huko mtakula mbele za BWANA, Mungu wenu, nanyi furahini katika yote mtakayotia mikono yenu, ninyi na wanyumbani mwenu, aliyokubariki BWANA, Mungu wako. 8 sifanye kwa kufuata mambo yote tuyafanyayo hapa leo, kila mtu kama aonavyo vema machoni pake;
Kumbukumbu la Torati 12:17-18 17 Usile ndani ya malango zaka za nafaka zako, wala ya divai yako, wala ya mafuta yako, wala wazaliwa wa kwanza wa makundi yako, ya ng’ombe wala ya kondoo, wala nadhiri zako uwekazo zozote, wala sadaka yako ya hiyari, wala sadaka ya kuinuliwa ya mkono wako; 18 akini hivyo watakula mbele za BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua BWANA, ungu wako, wewe, na mwanao mume na mke, na mtumwa wako mume na mke, na mlawi aliye ndani ya malango yako; nawe furahi mbele za BWANA, Mungu wako, katika yote utakayotia mkono wako.
Tunalishwa chakula cha kiroho kikamilifu sana kipindi hiki chote cha Sikukuu. Kwa wengi wetu hutuchukua miezi mingi hadi kufikia kuwaweka mahali pake na kuyaelewa yote yaliyokuwa yanafundishwa. Chakula cha kimwili pia kinatakiwa kiwe katika kiwango cha juu sana. Chakula cha kimwili kinatakiwa kiwe mahususi, cha kutosha, chenye kushinisha na chenye kuleta afya ya mwili. Mambo mengi mazuri sana na zawadi za masomo kumetokea kwa wapendwa kupeana kati yao wakati huu wa mazungumzo ya wakati wa chakula. Tunataka kuweka ukumbusho wa bwalo la chakula kama ni kitu mahususi na cha kukumbuka kama chakula cha kiroho.
Haturuhusiwi kula chakula hiki katika malango ya majumba yetu (Kut.23:17; Kum.16:16) isipokuwa ni katika ule mwaka wa tatu (Kum. 26:12), baada ya kutoa ile zaka yetu ya pili katika mwaka wa tatu wa mzunguko wa mwaka-wa-saba ambao unatolewa zaka maalumu ya kusaidia wajane na mayatima (Kum.14:28-29, 26:12-13). Maandiko matakatifu yanaturuhusu twaweza kula katika malango ya nyumba zetu katika mwaka wa tatu, lakini sio amrisho. Ikiwa wakiwepo ndugu, wapendwa katika maeneo yenu, inaruhusiwa kabisa kuadhimisha Sikukuu ndani ya malango ya nyumba yako katika mwaka huu wa 3. Wapendwa waishio katika hali ya utawanyiko wangejisikia ni vema zaidi kutunza sehemu ya zaka ya 2 ya miaka mingine, ili kwamba waweze kutunza na fungu la kutosha kuwawezesha kusafiri na kuadhimisha sikukuu na wenzao katika mwaka wa 3.
Mungu alitupa utaratibu huu muhimu wa kuhudhuria Sikukuu na kufurahia kula vinono na kunywa vinywaji vitamu (Neh. 8:10), na kwamba alitoa mfumo unaotoa hakikisho kwa watu wote waweza kuazimisha Sikukuu kama tukimtii.
Jinsi ya kuandaa Chakula Cha Sikukuu
Mungu ni Mungu wa sheria na utaratibu. Anafanya mambo yake katika uzuri na utaratibu (1Kor.14:40). Yeye ndiye mwanzilishi wa amani (1Kor.14:33). Kwahiyo, sisi pia tungepaswa kufanya mambo katika uzuri sana na katika utaratibu na kuwa na amani na kila tunachokifanya. Maandalizi ya chakula yanahitaji matayarisho ya kina ili kufanya Sikukuu iwe ya furaha zaidi kwa maeneo yote. Kwa kawaida Kanisa humwaagiza kila muumini kuandaa chakula kila makambi.ya Sikukuu. Ni kama ilivyo kwa kanini zote za maisha, hii inahitaji uandaaji, kupangilia, na maombi kama kitu cha muhimu sana. Sasa tutarudia kuona majukumu ya msingi kuyahusisha katika uandaaji wa chakula cha sikukuu.
Majukumu ya kila mmoja au ya pamoja
Jinsi kila kambi la Sikukuu linavyoandaliwa hutegemea na idadi ya washirika wanaohudhuria, upatikanaji wa vifaa, na malengo ya kila mmoja katika kuhudhuria kwake lile kambi. Kwa mfano, ikiwa idadi kubwa ya watu wanaokuja wakitokea maeneo mbalimbali, inaweza kuwa rahisi sana kwa mtu mmoja kuandaa orodha ya vyakula na kufanya sehemu kubwa ya manunuzi yake. Kwa hiyo wengine wanaweza kusaidia maandalizi ya chakula wakifika pale kambini na wakati wote wa kipindi cha Sikukuu. Uwezekano mwingine ni wa kuwaomba wanawake mbalimbali wafanye mipango kwa kuweka ratiba itakayo wawezesha kuhudumia chakula katika kambi kwa muda wa siku moja au mbili kwa ajili ya Sikukuu. Hii itawafanya wengine mioni mwetu ambao hawawezi kupika chakula cha watu wengi wajifundishe na kuendeleza kipaji hicho. Hii pia itasaidia kuendeleza na kuwafindisha waandaaji wa chakula kwa ajili ya makambi ya siku za mbeleni. Pia inahamasisha na kutia moyo watu kuweza kubeba majukumu na kazi kama timu ya pamoja iwapo mtu atatakiwa ashughulike na jambo la dharura. Mtu yeyote aweza kufanya kazi ya uandaaji kuhakikisha kuwa mipango yote ya orodha mbalimbali za kila siku zinakuja pamoja katika mintaarafu sahihi na utendaji ulio muafaka. Anaweza pia kusaidia katika kulinganisha ukubwa, orodha ya bidhaa zilizonunuliwa, na kwa utunzaji wa kumbukumbu kama zitahitajika.
Maafisa wa Kanisa watamchagua mhudumu wa mambo ya vyakula wa kila kambi. Wahusika wanaweza kupewa beji za wahudumu wa chakula.
Virutubisho na mlo kamili sambamba na Sheria ya Vyakula
Washirika wa Makanisa ya Kikristo ya Mungu wanaamini na kukubaliana na amri ya sheria ya vyakula kama ilivyoandikwa katika Mambo ya Walawi 11 na Kumbukumbu la Torati 14. Ili kujifunza vizuri kuhusu wazo la vyakula safi angalia jarida la Sheria ya Vyakula [015]. Hii kwa hakika ina maana tu ya kuwa ihakikishwe kuwa sheria za vyakula zinafuatwa wakati wa makambi ya sikukuu. Uangalifu wa ziada unatakiwa wakati wa kufanya manunuzi na kwa bidhaa zilizonunuliwa. Nembo nyingi zinazowekwa siku hizi zaweza kuwa na udanganyifu hivyo zinahitaji ukaguzi maalumu kwenye mchanganyo wa makasha ya keki, mafuta ya kupikia, peremende (au bisikuti), mikate na maharagwe ya kwenye makopo. Kuna wakati fulani iliwahi kutokea kuwa katika makopo yenye chapa inayoelezea kuwa na nyama ya bata-mzinga iliyotengenezwa Marekani lakini ilichanganywa pamoja na nyama ya nguruwe; hivyo basi ikawa imenajisiwa. Inatakiwa awepo mmja wapo atakayekuwa makini sana wakati wengine wakiwa wanamsaidia katika manunuzi wakati mwingine wanasahau kuangalia na kusoma nembo zake. Kwahiyo, ni muhimu na inasaidia sana kusoma nembo hizi wakati bidhaa hizi zinapoletwa jikoni ili kwamba kama vilikuwa havijachunguzwa sawasawa vilipokuwa kwenye ghala za vyakula.
Tunaadhimisha siku za Mikate Isiyotiwa Chachu (Kut.12:8, 19; 13:3; 34:18; Kum.16:1-8). Wakati wa Mikate Isiyotiwa Chachu ni mlo ambao wajibu wa muandaaji kuwa ni aina ya mikate isiyo na chachu ndani yake tu ndiyo inatumika wakati wote wa Sikukuu hii. Tumeamriwa kuila mikate isiyotiwa hamira ndani yake katika kipindi hiki cha siku saba (Kut.12:15; 13:3; 34:18; Kum.16:3, 8). Kwa maelezo zaidi kuhusu kuhusu mambo ya kufanya kwa kipindi hiki soma jarida lisemalo Mambo ya kufanya Katika Siku ya Mikate Isiyotiwa Chachu [R2]. Pia ni wajibu wa mwandaaji wa kambi kuhakikisha kuwa aina zote za mazalia ya hamira au chachu zimeondolewa kabisa na zisiwepo katika eneo la jikoni kabla ya giza halijaanza jioni ya siku ya 15 ya mwezi wa kwanza (Kut.12:15, 19; Kum.16:4). Anapaswa kabisa kuhakikisha kuwa hakuna masalio yoyote ya chachu au mazalia ya hamira kuliwa na watu wa Mungu wakati huu wa Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu.
Chakula kinapaswa kijumlishwe na aina mbalimbali ya nyama safi, mboga za majani, matunda, mboga za nafaka, na jamii yote ya vitu vya maziwa.
Juisi za matunda zinatakiwa ziwepo wakati wote na kwa watu wote, hususan watoto.
Aina ya vileo inaruhusiwa kama jukumu la kila mmoja kwa ujumla, na watakaomudu kununua waweza kuwanunulia na wengine wasioweza kununua. Hili ni jukumu la mtu binafsi.
Mwandaaji wa chakula vilevile kuwa wote wanapatiwa chakula wakati wote wa Sikukuu. Kwa wakati huu wote hii inahusiana na kutoa chakula kwenye kibakuli iwapo kama mhusika hayupo kwa sababu ya anaumwa. Msimamizi wa shughuli za chakula anatakiwa pia awe na uwezo wa kujibu maswali yoyote kuhusiana na vitu vilivyoandaliwa iwapo kama kunamatatizo ya vyakula vyenye kudhuru mwili, nk. Washiriki wanaombwa kumshauri msimamizi wa mambo ya chakula hitaji lolote maalumu siku kadhaa kabla ya Sikukuu.
Maandalizi na usimamizi
Tunaamini kuhusu kumtii Mungu na Sheria zake; kwahiyo hatufanyi-kazi au kununua au kuuza siku ya Sabato (Hes. 13:32-36; Neh.10:28-31, 13:15-21; Yer.17:21-22).Hali hii vilevile inaendelea wakati tunapokutanika pamoja kwa Sikukuu. Kwahiyo, uangalifu na umakini unahitajika vinatakiwa sana kupewa hizi Sabato au Sabato za kila wiki. Hii haijawahi kamwe kutokea kuwa imesababisha matatizo katika historia, kinachotakiwa ni kuafanya mpangilio yakinifu tu wa orodha ya vyakula na manunuzi sawasawa na mahitajio. Wakati huu wa Sikukuu tunatakiwa kuandaa chakula zaidi zaidi ya vile tunavyozoelea kuwa navyo majumbani mwetu tuwapo na familia zetu kwa kawaida, lakini hatimaye tutakuwa na watu wengi zaidi watakao tusaidia kufanya maandalizi.
Katika ukurasa wa jarida shirikishi utaona mfano wa orodha ya wahudumu wa kujitolea iweje. Orodha ya majaribio na ya wanaojitolea yaweza kubandikwa katika meza ya maelezo. Pia inasaidia sana kama nakala yake itabandikwa jikoni. Ni jambo la busara sana kueleza kwenye tangazo hili kuwa hawa ni wa muda na kuweko zamu za mabadilishano. Wakati mwingine kunaweza kuwepo na mtu ambaye hawezi kula kiasi cha nyama kwa wingi unaohitajika nk. Mwingine atatkiwa awe ajifanye rahisi na kufanya marekebisho pale inapowezekana. Kwahiyo basi, kama mwandaaji wa chakula au msimamizi wa kila siku akiwa hayupo kwa masaa fulani nje, wajisikie huru kumuomba mtu mwingine yeyote kuchukua usukani wa kazi ili kuwafanya watu wa Mungu wapate chakula kinachohitajika kwa wakati ule.
Inaweza kuwepo kazi kwa yeyote anayependa kutoa msaada. Msimamizi wa vipindi wa kila siku anatakiwa azoee shughuli za kila siku na na kupangilia mambo kazi bila kukosea. Kwa mfano, kama mzee wa kike anapenda kumsaidia, muombe afanye kazi ya kutayarisha viungo au chochote anachoweza kufanya kukaa tu chini mwili haupendi. Au kama mtu anayetaka kusaidia anatumia kiti cha walemavu, mpatie vitu anavyohitaji kuvifanyia kazi na umpitie pitie kuona kama atahitaji vingine zaidi. Kwakweli sisi sote tu familia moja ya Mungu na wote tu sehemu katika Mwili wa Kristo. Tunatakiwa kupendana na kutumikiana kama ndugu na kujaribu kuwa na masaidiano katika maandalizi na kufanya usafi kadiri iwezekanavyo. Vijana na chipukizi walio kwenye rika la miaka kumi na tatu kwenda juu wanaweza kutumika vizuri sana kwa shughuli za ubabaji wa vitu na kugawa kwa watu husika kwenye maeneo yanayopatikana vinywaji. Baadhi ya jioni watu wazima wanaweza kujitoa kusaidia kazi za uokaji wa mikate na vyakula aina ya makande vinavyofaa kutumiwa kwa milo ya mchana na jioni siku za Sabato. Ili kuongezea aina ya mabadiliko ya vyakula kwa nyakati mbalimbali wanaume wanaweza kuombwa wachune nyama. Kuishi pamoja kama ndigu muda wa siku 8 ni tendo la baraka za ajabu sana na kina thawabu kuu sana wanapokuwa wote wanashiriki kwa kuifanya Sikukuu iweze kufana. Kama kutatumika jiko la biashara au la kisasa itakuwa ni muhimu kwa wale wote wanaoshughulika na mambo ya chakula wafundishwe na wathibitishwe kwa usafi wa chakula na uagwaji. Kwa hiyo, ni jambo muhimu sana kwa yeyote anayetaka kusadia kazi za jikoni kuhudhuria kozi inayotambulika katika nchi yao. Hata licha ya mafunzo haya kuwa ni sharti la utumiaji wa vifaa vya jikoni katika nchi husika, hii ni huduma kwa wapendwa kwa ujumla kushiriki kwako kozi hizi, nah ii itazuia aina yoyote ya hasara kwa mipangilio muhimu ya kanisa.
Kanuni za Nchi za Chakula, Karantini na Afya
Kila nchi imejitungia sheria zake za mambo ya vyakula ambazo zinatumika katika nchi au jimboni mle ambako Sikukuu inafanyika.
Sisi tunashikilia sheria ya karantini kama inavyoelekezwa na kitabu cha Mambo ya Walawi 13:45-40 na Hesabu 5:1-4. Hata kama mtu yupo katika ratiba ya kuhudumia au ya kusaidia maandalizi ya chakula. Iwapo kama yeye mwenyewe au mtoto wake anaumwa, basi asisaidie kabisa kazi ya maandalizi ya chakula. Hii pia inaendana pamoja ya uhudhuraji wake katika ibada. Na iwapo kama kuna iana yoyote ya hatari za magojwa ya kuambukiza kwa mtu yeyote, tutapaswa kujitenga hadi atkaporudia hali ya kupona.
Bajeti
Tunamwabudu Mungu kwa kudumu katika kutaniko lake lililoamriwa (Kut.23:14, 34:22-24; Kum.16:16). Mpango wa Mungu ni kufungua mlango wa mapato kwa kila mshirika binafsi ili aweze kuhudhuria Sikukuu. Kila mshirika binafsi anatakiwa kutunza kwa uaminifu wake wote na kusimamia zaka yake ya pili kwa mzunguko wa mwaka wa saba (Kum. 14:22-23). Kwa kufanya hivi tutaweza kuwa tayari kuhudhuria Sikukuu za Mungu katika mwaka wa tatu na wa saba wakati tutakapokuwa hatuna hatuna “zaka ya pili ya kila mwaka”, katika mwaka wa tatu zaka yetu ya pili inaunganishwa pamoja na ile Zaka ya Mwaka wa Tatu ambayo ni kwa ajili ya wajane na mayatima (Kum.14:28-29, 26:12-13). Angalia Kalenda ya mpangilio wa utoaji zaka wa Makanisa ya Kikristo ya Mungu. Kwa-hiyo, tunapaswa kupangilia na kutunza akiba yetu ya zaka ya pili ili kuhakikisha kuwa tutaweza kuhudhuria Sikukuu ili tuwe watendakazi waaminifu. Ni vizuri kusaidia zaka yetu ya pili katika akaunti nyingine mbali na zile zinazotia riba (Kut.22:25; Law.25:36; Kum.23:19-20).Asilimia 2 ya Bathi ya Mafuta, ambayo tunaamriwa kuhifadhi, inaweza kuongezwa katika zaka yetu ya pili (Eze.45:14-17). Kwa maelezo zaidi kuhusu Bathi ya Mafuta, soma jarida linalosema Ujumbe wa Sabato Sehemu B. ya tarehe 12/5/26/120 wa James Dailley au http://www.ccg.org/_domain/ccg.org/Sabbath/2003/S_08_09_03b.htm na jarida linalosema Utoaji wa Zaka [161] na jarida la Ijumaa Maandalizi ya Sabato [285]. kwa maelezo zaidi kuhusu zaka ya zaka katika Nehemia 10:38, soma jarida la Katiba [A2] na Utoaji wa Zaka [161].
Ingawa watu wana zaka yao ya pili na Bathi ya Mafuta kwa ajili ya kuhudhuria Sikukuu, hii bado ni fedha iliyotengwa na Mungu kwaajili ya kila mtu ili ahudhurie Sikukuu. Ni wajibu wa mwandaaji wa chakula kuhakikisha kuwa chakula katika siku ya Sabato kina ubora unaotakiwa kwa siku ya Sabato na milo ya siku siku za kawaida za Sikukuu vilevile kiwe na mahadhi yanayotakikana. Lakini kuna ukweli wa kuweka mlingano hukuna kule katika kila jambo. Baadhi ya milo itatakiwa kuwa na gharama kidogo ifaayo kuweka mlinganisho tofauti na gharama za chakula cha mlo unaoandaliwa kwa siku ya Sabato au aina nyingine zaidi ya ya milo yenye gharama zaidi.
Kwa baadhi ya watu wa Mungu, zaka yao ya pili haiwezi kutosha kuchukua gharama zote za usafiri na malazi kwa vile zilivyo ndogo, nab ado hatuja sema lolote kuhusu uwezekano wa bajeti ya chakula. Gharama za mlo ktika Sikukuu nchini Marekani ni wastani wa US$ 7.00-10.00 kwa mtu mzima. Sisi hulipia gharama za wale wote walio chini ya umri wa miaka ishirini kwa jinsi tunavyowatoza watu wazima. Katikati ya Sikukuu tangazo linafanywa kuelezea kuhusu gharama za chakula. Kumbuka kuwa tunapaswa kutoa kile tulichoweza kutoa, ili kufidia bajeti ya chakula. Maskini watakuwepo siku zote (Mat. 26:11; Marko 14:7; Yohana 12:8). Kwa hiyo, kama kuna mtu anacho cha zaidi na anapenda kusaidia kufidia gharama za wale wasio na fedha hiyo itakuwa baraka sana. Matajiri wanatakiwa wawe wakarimu kwa masikini (Kum.15:7-11). Kanisa kitafidia kulipia gharama za chakula ikiwa tumepungukiwa kabisa jinsi ya kulipa deni, lakini ni vizuri zaidi kama tutaweza kujisaidia kulipia gharama zetu kuliko kuchukua kilichotolewa kwa ajili ya kuendeleza Injili ili kulipia gharama za deni la chakula.
Kuhitimisha au Kufunga
Ni jambo la baraka kiasi gain kujihudhurisha mahali pale ambapo Mungu amelikalisha Jina lake ili tukajifunze, tukamuabudu, na Kumuishia. Hebu basi na tujitahidi kuadhimisha Sikukuu kwa moyo wa kweli, na wakati wote tupende kutumikiana, kusaidia kazi kwenye Sikukuu katika hali ya kufurahia na kupeana zawadi. Hebu basin a tuone kuwa ni jambo la baraka sana kuwa ni miongoni mwao waliochaguliwa na Mungu wanaozishika na kuziishia sheria za Eloah uaani Mungu.
Nyongeza 1
Binafsi
Jitahidi uwe na orodha ya wahudhuriaji. Msimamizi wa kambi lazima ajue ni yupi amuone yanapotokea mambo ya dharura. Au pengine waweza kutumia vitambulisho vya dharura?
Idadi ya watu wazima:
Idadi ya watoto:
Eneo Wanakolala: [mkuu wa maandalizi lazima ajue ni nani anayeishi kwenye chumba gain, nk. Hii ni kwa ajili ya mambo ya dharura yanapotokea kama vile mlipuko wa moto, nk]
Vitambulisho vya fedha, hundi, hundi ya msafari, fedha za dharura nk..
Ramani ya eneo la kambi.
Vitu vilivyo muhimu kuwekea vigezo katika kumwelezea mtu kambi ilipo.
Huduma ya mlango wa dharura kwa mashiriki kama upo.
Mkataba wa upangaji na ukumbi. Pengine watu 2 watahitaji nakala kwa wakati mmoja wao anapokuwa hayupo.
Nambari ya Simu (ya mkononi) ya dharura na nambari za wandaaji wote na ikiwezekana za mashemasi.
Malalamiko yote yahusuyo malazi: yapelekwe moja kwa moja kwa Mkuu wa maandalizi kama yanaonekana hayawezi kutatulika kiurahisi na wahusika wa eneo.
Mwishoni mwa kipindi cha makambi, liweke eneo katika mazingira mazuri kwa ajili ya matumizi ya kipindi cha makambi yanayokuja.
Shughuli ya Kuchukua watu Uwanja wa Ndege au kwenye Vituo vya Mabasi
Andaa ratiba
Jua ninani
Wakati gain
Wapi
Na nani
Mahitaji Muhimu; aina hii ya taarifa ya umakiniinatakiwa itolewe kwa kila mtu kwa ajili ya mahitaji yasiyo na chanzo chake. Mkuu wa maandalizi atatkiwa kujua kama kuna mtu ametafuta msaada wa kifedha za kuhudhuria kambi ya Sikukuu ili ahakikishe kuwa mahitaji yake yakefikiwa.
Kabidhi kazi hiyo kwa washiriki husika kwanza kwenye Sikukuu ili kuweka uhakika kuwa watakuwa na muda wa kutosha kujiandaa vizuri, k.m. kuleta orodha ya maombi, kuandaa mahubiri, kuweka sawa mawazo ya watoto hasa hasa kwa ajili ya Ashirika wa Meza ya Bwana.
Bandika tangazo la orodha ya watoa huduma wa kujitolea kwenye ubao wa matangazo utakaosomwa kirahisi na wengi ili kwamba yeyote anayapenda aweze kujiandikisha jina lake kwa ajili ya shughuli ziliyopendekezwa, k.m kusaidia jikoni, kuweka mipangilio & kusafisha fanya maeneo, kuwasaidia wandaaji kwa shughuli yoyote ile
Ukumbi wa mkutano
Jozi ya Vyombo vya Muziki.
Ikiwezekana andaa vipaza sauti 2 kwa matumizi ya masomo ya Biblia ili kwamba wale walio na matatizo ya kusikia waweze kushiriki wakisia na kuelewa kwa urahisi. Inaweza pia kurekodiwa kwenye kanda ikionekana inafaa.
Mengine
Uandaliwe ubao wa matangazo au meza
Uandikwe Amri Kumi za Mungu na zibandikwe
Ratiba ibandikwe kwa ajili ya watu watakao ingia kwenye zamu za kutoa huduma mbalimbali, Masomo ya Biblia na eneo la kulia chakua na muda wa chakula.
Chumba cha wamama
Jozi ya vyombo vya Muziki
Mabunda ya karatasi laini za chooni, taulo na tishu
Vitu vya kula na kuchezea watoto kama masomo yanaonekana kufanyika katika chumba hichohicho kimoja
Maji na juisi za watoto (na vikombe vya kunywea)
Vifaa Muhimu Kuwanavyo
Kanda tupu za kurekodia
Vyombo vya kuchukulia umeme (yaani surge bar na extention cords yake)
Taa ya mezani ikiwa mwanga ni dhaifu kwenye chumba hicho
Kitambaa cha mezani kama mnenaji atahitaji (leta pini zilizo salama za kufungia hiki kitambaa)
Ubao mkavu wenye kufutika (mweupe) wenye kuhamishika na kifutio chake
Waweza kufunga madirisha kama utakuwa unatumia AV au kama italazimika wakati wa kushiriki Meza ya Bwana kwa ajli ya kuosha miguu.
Ubao au meza ya Matangazo
Ramani ya mahali kambi ilipo kukijumlishwa vitu vilivyo karibu yake kama vile zahanati, maelekezo na simu kituo cha Polisi, simu na maelekezo yake. Mwelekeo wa kambi lilipo, yajumlishe anuani na simu.
Kikasha chenye mambo mbalimbali: kama vile rula, mkasi, kibania-karatasi, vipini na kitubu
Tarumbeta za Pembe au za Fedha
Nakala ya Kitabu cha Ukiri wa Imani, Kalenda ya Mwaka, Katiba; (au vifungu vya maandiko matakatifu k.m.Washika Sabato wa Transylvania); orodha ya majarida ya masomo yaliyoko, kanda za kunasia sauti, nk.
Vingine vinavyo hitajika
Ratiba ya Wahubiri
Ratiba za matukio kama zitakuwepo
Orodha ya wanaohudumia jikoni au kwenye ukumbi
Orodha ya mawasiliano kwa taadhari ya mambo ya dharura yakitokea kwemye Sikukuu. Pengine hata orodha ya kila mtu kwa kila siku za Sikukuu kwa hadhari ya kama mtu anaweza kuhitaji huduma ya upako wa mafuta, nk.
Kwenye Ibada
Tayarisha kitu cha kuwekea maji au bilauri kwenye meza ya wahubiri.
Tayarisha vitafunwa vidogovidogo viwepo wakati ibada inapochukua muda mrefu au mtu anaweza kuhitaji viwepo kwa ajili ya kushusha kiwango cha shinikizo la damu, nk.
Weka maji na vikombe nyuma ya ukumbi kwa ajili ya wanaohitaji.
Tayarisha karatasi, taulo na makaratasi laini yawepo sehemu ya wazi kwa tahadhari ya wanaotaka kuzitumia.
Kuwe na Vitabu vya Nyimbo & muziki hata kwa njia ya kanda, CD, au nyimbo za kuimbwa na watu kama mpiga piano atakuwepo.
Andaa wimbo maalumu kama ikiwezekana.
Andaa mpiga Tarumbeta au Shofa.
Andaa watakao ongoza uimbaji na msimamizi wa matangazo.
Mwandae mtua atakayekuwa akigawa karatasi za matangazo.
Mpange mhudumu wa muda kama wahubiri watamhitaji.
Vifaa vitakavyotakiwa kwenye Masomo ya Biblia
Biblia Husika inayotumika katika nchi yako (hasa Companion Bible)
Maandiko Mwongozo (Interlinears)
Kamusi ya Biblia (Lexicon)
Itifaki ya Biblia (Strong’s Concordance)
Kamusi ya kawaida (Dictionary)
Kuwe na Biblia zenye tafsiri na matoleo mbalimbali (kwa kawaida watu huwa na Biblia za matoleo mbalimbali).
Toa vifaa vingine vyenye kusaidia kuyapitia maangiko kama itakavyo hitajiwa na Mwandaaji wa Sikukuu.
Vifaa au vitu vyenye kutumia umeme:
Mashine ya kurudufia nakala za masomo (Dubbing Machine) kama itahitajika na Mwandaaji wa Sikukuu.
Vifaa vya kusafishia mashine kama itatumika sana
Mashine ya kurudufu (Laptop) na kutolea chapa (Printer) kama zitahitajika
Utaratibu wa vipindi vya Biblia iwapo kama kazi ya marudio itahitajika kufanywa
CD ya karatasi kama compyuta itakuwepo
Piano au kinanda kama vitahitajika
Deki za TV/VCR/DVD kama vitatakiwa
Mashine kubwa ya kurudufia nakala (Photocopy) itatakiwa iwepo katika maeneo hayo kama italazimika kuwa hivyo, lakini jarida kwa ajili ya Sikukuu zinatakiwa ziandaliwe mapema kabla yake kwa kiasi cha nakala za kutosha na ziletwe kambini na Mkuu wa maandalizi ya Sikukuu na/au wale waliochapangiwa kwa kazi hii.
Bwana mitambo wa jozi ya vyombo vya muziki lazima awe na uzoefu na vifaa vinavyotumika. Wahubiri watamuarifu mhusika wa wahusika kama watahitaji warekodi na/au waandae mikanda, hususan kama ule ubao mweupe au chombo kingine kitakuwa kinatumika na wahubiri hawa, k.m. maigizo au onyesho la utelezaji, nk.
Masharti ya Nyongeza kwa Sikukuu Yenyewe
Siku ya makusaniko:
Kutapinwa baragumu ya fedha na/au ya Kondoo mume
Bahasha za sadaka zenye nembo maalumu
Kikapu maalumu cha kukusanyia bahasha
Pasaka/Meza ya Bwana
Andaa beseni/taulo-ni jukumu la kila mmoja
Viti vya watoto wachanga-andaa mapema kabla ya muda wa kuanza
Divai na chombo cha kufungulia
Bilauri za divai na sinia lake
Mkate Usio na chachu ndani yake (ngano, mafuta chumvi) na sinia zake
Kitambaa cha mezani kikubwa na kidogo
Weka watu watakaohudumu na kusafisha sinia za mikate na vikombe vya divai na kuondoa mkate au divai yoyote isiyotumika
Usiku wa Kuangaliwa:
Mnyama aliyeokwa kutoka katika kundi la mifugo yako (sio na mifupa) atapikwa kambini.
Mboga zenye uchungu kama mchunga zitaliwa
Kipindi maalumu cha watoto kuuliza maswali (Kut.12:26); ruhusu watoto waulize mwaswali yao wenyewe vilevile.
Divai kwa watu wazima (na juisi kwa watoto na kwa yeyote atakayependa).
Kiandaliwe kisu kikali kiwepo.
Mkate Usiokuwa na Chachu yaani hamira uandaliwe
Ibada ya Mganda wa Kutikiswa: Ibada hii huanza milango ya saa 3:00 Asubuhi.
Viandaliwe vitafunwa baada ya saa 3:00 Asubuhi, na saa lingine la kujifunza neno inaonekana itakuwa vizuri zaidi.
Ibada ya Pentekoste: Huanza saa 3:00 Asubuhi (Kwa kuzingatia Huduma ya Masaa ya Mchana).
Maelekezo ya hapa ni sawa tu na ya kwenye orodha ya siku ya makusanyiko
Viandaliwe vitafunwa baada ya ibada ya kwanza kisha masomo yataendelea na chakula
Sikukuu ya Vibanda
Rudi kwenye maelezo ya orodha ya Siku ya Makusaniko
Ukaguzi wa Jikoni
Bandika tangazo la orodha ya mambo
Bandika tangazo la orodha ya watakaofanya kazi za kujitolea
Weaka orodha ya vitu vilivyonunuliwa dukani mahala palipo wazi jikoni. Hii itawazesha kumfanya mtu yeyote apitaye huko akiona bidhaa zinapungua idadi akaenda kuongezea kwenye orodha.
Wakati wa maandalizi ya chakula:
Wakati wote safisha mikono kwa sabuni na maji.
Vaa sokisi safi za mikononi za plastiki na uwe unazibadilisha katikati ya kazi.
Vuta nywele zako ndefu kwa nyuma kasha uzibane kwa kibanio ili zisiyumbeyumbe; tumia kibandiko kama kipo kuzizuia.
Maandalizi ya nyama na ugawaji
Tumia ubao wa kukatia katika maandalizi au anza kukata nyama juu yake. Kama ubao huu wa kukatia haupo, basi tumia ubao mwingine unaofaa kwa nyama na mwingine kwa mboga za majani na matunda. Kipimajoto kitumikacho wakati wa upishi wa nyama vilevile kitumike wakati huu wa mapishi.
Chakula cha moto kinaweza kuhifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhi joto la chakula au kwenye jokofu ikiwa ni muhimu.
Gandisha vitu vyote kwa haraka.
Uhifadhi wa Chakula:
Inabidi vyakula vibandikwe nembo na tarehe zake.
Vyakula vikikaa zaidi ya siku 3 itabidi vitupwe jalalani.
Vyakula vinaweza kutunzwa kwenye jokofu na kugandishwa ili kuviongezea uzima visioze.
Uoshaji wa vikombe
Uataratibu wa kuvipisha vyombo kwenye bwalo la kuoshea mara 3 unafaa utumike mara zote: mara ya kwanza zamisha kwenye maji moto yenye sabuni, mara ya pili tia kwenye maji safi kasha usuuze, utiaji huu wa mara ya tatu utachanganywa na dawa zinazozuia maambukizo ya vijidudu. Dawa hii ya kuua vijidudu inaweza kutiwa kidogo tu kiasi cha kama kijiko 1 tu cha chai kwa kila galoni mbili za maji.
Vizulia vya mezani na meza zenyewe za kulia zinabidi zipanguswe kabla na baada ya kutumiwa.
Takataka ziaondolewe kila mara zinapoonekana zipo kwa wingi na kwa kila mwisho wa kila siku. Ni vizuri kuweka makasha ya takataka sehemu zinazopitika na wengi kwa kuwa makasha haya ya takataka ni rahisi kuyabeba.
Vifaa: hakikisha kuwa vifaa vyote maka vile jiko la mafuta, makopo ya kahawa, nk. View vimefungwa kabisa, hasahasa kunapofikia mwishoni mwa siku. Kama unatumia birika la ugongo nk, yanye kutumia umeme hakikisha kuwa ukiweka kwenye waya basi uwe unatumia usiweke tu kikiwa hakitumii umeme. Wakati mwingine watu wanajaribu kuzima umeme kwenye majiko na kwingineko kwa nia nzuri tu ya kusaidia wakati ambapo viliwashiwa kutumia umeme kwa sababu fulani muhimu.
Cha Msingi Kukumbuka:
Kama ilivyoelezwa huko nyuma kuwa watu wanaohusika na masuala ya chakula kwenye Sikukuu lazima wawe na cheti mhudumu chakula kinachokubalika au kitambulisho chenye sifa inayokubalika kulingana na viwango vilivyowekwa katika jimbo au taifa lile. Mtu yeyote asiyekuwa na sifa hizi atafanya kazi ya usaiizi tu ya jikoni chini ya uangalizi na maelekezo ya yule mwenye sifa za cheti kama tulivyo muelezea hapo juu.
MWISHO!
q