Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[233]
Je, Ni Eliya?
(Toleo
La 2.0 19971220-20080203)
Jarida hili linaelezea dhana ambayo imewekwa au kufundishwa kwenye baadhi
ya makanisa fulani fulani ambayo ilikuwa inaminisha watu kumuona na kuamini
kwamba Herbert W. Armstrong alikuwa ni Eliya na kwamba mwanae, Garner Ted
Armstrong, au aliyemrithi baadae, Joseph W. Tkach, kwamba ni Elisha.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hati Miliki © 1997, 2008 Wade Cox)
(Tr. 2014)
Masomo haya
yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu
bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni
lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa
nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa
kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Je, Eliya?
Mmoja hakuweza
kusaidia, lakini kumbuka kuwa barua iliyoandikwa kwenye makala ya Jarida: Habari za Makanisa ya Mungu [The
Journal: News of the Churches of God, Vol. I No. 10 (21 Nov. 1997)], inaelezea
jambo ambalo ni la kutatanisha na kukanganya kwa namna fulani likifundishwa kiubezaji
mkuwa na huduma ya Kanisa laWorldwide Church of God kwamba Herbert Armstrong alikuwa
ni Eliya. Waumini walikuwa wakifundishwa pia kwamba Garner Ted Armstrong alikuwa
ni Elisha na kudhani alipaswa apewe yeye. Kisha waumini walikuwa wakifundishwa
kuwa inadhaniwa ilikuwa imeondolewa kutoka kwa Joe Tkach, ambaye alikuwa ni
Elisha. Huduma iliyosema hivi mara nyingi iliwakanganya watu na kuwaletea usumbufu
mkubwa na walipokuwa wakiyasema maneno haya hata makoo yao yalikwaruzika
kusikika, jambo ambalo lilikuwa ni upuuzi wa wazi na dhahiri.
Wakati umefika wa
kuondoa dhana hii potofu nay a uwongo mioyoni na kuitokomeza kabisa, tukitaraji
kufanya hivyo mara moja na kwa wote, kwenye mioyo ya watu wanaodhani na kuamini
hivyo waliobakia Makanisani na kutuzuia sisi kutokana na mkanganyiko mwingine wowote
kwa madai yanayoingizwa kutoka kwa watu wengi waliosafishwa akili zao makanisani.
Ahadi ya Mungu
1. Eliya alipaswa
kuja na kuyarejesha mambo yote (Malaki 4:5-6).
2. Kristo alisema
kuwa Eliya angekuja hakika na kuyarejesha mambo yote. Alisema pia kwamba
alikuwa ameisha kuja tayari, na alimtaja Yohana Mbatizaji. Kwa hiyo Eliya ajaye
alitanguliwa na aina-ashirio.
Kipimo: Iwapo
kama Herbert Armstrong alikuwa ndiye Eliya, basi angekuwa amerejesha mambo yote.
Bali alifariki na kwa hiyo kazi zake zimeishia hapohapo. Yeye mwenyewe hana la
kufanya zaidi hadi atakaposimama kwenye Ufufuo wa Kwanza au wa Pili wa Wafu,
wowote ule miongoni mwake ambao kwao atajikuta ameamshwa na kusimama ndani yake.
Kama tutakiona
kitu kimoja aambacho hajawahi kukirejesha, ndipo hatupaswi kumlinganisha au kumchukulia
yeye kwa kumfananisha na Eliya ajaye, kama ambavyo hakuwa hivyo kwa kweli, na
kama angekuwa ni yeye, basi angekuwa amekwisha yarejesha mambo yote.
Kwa sasa ni upotoshaji
kudai kwamba alikuwa kwenye mstari wa kuyarejesha mambo yote. Hoja hiyo haiwezi
kukubalika wala kuingia akilini mwa mtu yeyote kwenye Kanisa tangu zama za
Kristo na Mitume waliokuwepo katika karne ya kwanza na kuendelea.
Mfano wa Jaribio wa 1: Fundisho kuhusu Yubile
Utekelezaji na
utendaji wa mfumo wa kibiblia wa utoaji wa zaka zote mbili na Torati unaendana
na mzunguko wa miaka ya Yubile. Hakuna mahali palipowahi kudaiwa kabisa na Herbert
Armstrong au huduma yake kwamba alishagawahi kurejesha fundisho la Yubile na
utaratibu wake. Baadhi ya watumishi wake walijua na kukubali kwamba namna na jinsi
mgangilio wa Yubile ungewekwa na kurejeshwa, lakini bado hakuna hata mmoja wao
aliyejaribu kufundisha au kuwaelekeza watu kuhusu utaratibu huu wa Yubile na
kuwafundisha waumini na wala kuthubutu tu kuurejesha utaratibu huu (soma jarida
la Maana ya Maono ya Ezekieli (Na.
108)).
Kwenye mfumo huu
unaoendena na usomaji kikamilifu wa Torati na pia utaratibu wa utoaji wa zaka
(soma jarida la Utoaji wa Zaka (Na. 161)). Kile kilichoanzishwa na kuchukua mahala pa
Yubile kilikuwa ni mzunguko wa bandia wa miaka mitatu mitatu unaotokana na
kipindi cha kubatizwa kwa mtu, na kila mtu alifundishwa kutoa zaka kwa msingi
wa kila miaka mitatu mitatu. Utaratibu huu ni kinyume sana na Maandiko Matakatifu,
ambayo yanatutaka au kutuamuru ‘kutoa zaka hii ya mwaka wa tatu’ kwenye kila
mwaka wa tatu tu ulio kwenye mzunguko wa miaka saba. Zaidi ya yote, ni kwamba
mwaka wa saba haukuwa ni mwaka wa kutoa zaka kwa mujibu wa Torati. Kwa hiyo, Herbert
Armstrong sio tu kuwa hakurejesha mfumo na mzunguko huu wa Yubile, bali pia
aliwafundisha watu kupinga jambo hili na kuwaamuru watumishi au wahubiri wake
wafundishe mafundisho ya kupinga jambo hili. Kwa jambo hili tu peke yake,
anakosa kigezo cha yeye kuwa Eliya.
Mfano wa Jaribio wa 2: Usomaji wa Torati
Kwa mujibu wa
Torati yenyewe, Torati yote inatakiwa isomwe kwenye Sikukuu katika kila miaka
saba, katika mwaka wa saba ya mzunguko wa Yubile. Hii ilianzia kutoka kwenye
Sikukuu ya Ukumbusho wa Baragumu iliyoandaliwa na kina Ezra na Nehemia, na
kwenye Sikuu ya Vibanda. Hii ilifanywa kwa wazi sana na kina Ezra na Nehemia
sawasawa na ilivyoagiza Torati wakati walipokuwa wanafanya marejesho (Nehemia
8:1-18; pia soma jarida la Usomaji wa Torati wa Ezra na Nehemia (Na. 250)). Maagizo haya ya Torati yanapatikana
kwenye Kumbukumbu la Torati 31:9-12 (pia soma mlolongo wa majarida yanayoielezea
Torati, Nambari 252-263). Hii haikufanyika kwenye huduma ya Herbert
Armstrong. Na wala hakufanya marejesho ya jambo hili lililoamriwa na Torati, na
kwa ajili hiyo anashindwa pia kufikia vigezo vya yeye kuaminika kuwa ni Eliya.
Mfano wa Jaribio wa 3 na 4: Miandamo ya Mwezi Mpya na Kalenda
Isaya 66:23 inasema
wazi sana kwamba maadhimisho ya Siku za Miandamo ya Mwezi Mpya yatarejeshwa
kwenye marejesho ya mwisho ya mambo yote (soma majarida mengine kadhaa
yanayoelezea Miandamo ya Mwezi na pia jarida la Kalenda ya Mungu (Na. 156)). Na kwa hiyo, uelewa juu ya jambo hili ni lazima uwe ni sehemu marejesho ya
mwisho. Maadhimisho haya ya Miandamo ya Mwezi Mpya hayajafanyika wala kurejeshwa
na Herbert Armstrong. Alijaribu tu kufundisha kwenye masomo yake ambayo ni
mafundisho ya Biblia ya jioni kuhusu Miandamo ya Mwezi katia siku za mwanzo wa
huduma yake, lakini alikata tama na kuachana nayo baadae. Kwa kweli, masomo
hayo ya Biblia yalikuwa yanafanyika katika siku zilizoendana sawa na kalenda ya
Hileli, ambayo tunajua kuwa ikitumika katika kipindi cha Kristo na haikuwa ni
kalenda iliyotumiwa na Kristo au Yohana Mbatizaji katika kipindi cha Hekalu.
Kwa hiyo, kwa
sababu hizi mbili hawezi kuwa ni Yule Eliya ajae, kwa kuwa hakuweza kurejesha
maadhimisho ya Miandamo ya Mwenzi wala kuifuata lakenda sahihi iliyotumiwa na
Kristo na Eliya aliyekuja kimfano, ambaye ni Yohana Mbatizaji. Inafuatia kwamba
Eliya ni lazima awe anaifuata kalenda ileile na mfumo kama wa watangulizi wake
na Masihi.
Mfano wa Jaribio wa 5: Kuhusu Sadaka
Eliya ni lazima
atarejesha utaratibu na mfumo sahihi wa utoaji sadaka. Kuna utoaji mara tatu wa
sadaka zilizoamriwa kutolewa kila mwaka: kwenye maadhimisho ya Pasaka, idi ya
Majuma au Pentekoste na Mkutaniko wa Sikukuu ya Vibanda. Hizi zinatakiwa
zichukuliwe mwanzoni mwa maadhimisho
haya ya Sikukuu na zisiachwe zimebakia hadi asubuhi (Kutoka 23:14-19). Soma pia
jarida la Utoaji wa Sadaka (Na. 275).
Herbert Armstrong
wala hakufanya hivi. Bali alianzisha utaratibu wa kutoa sadaka mara saba kwa
mwaka badala ya mara tatu, kwa sababu hii hanasifa za kumfanya astahili kuwa
Eliya.
Mfano wa Jaribio wa 6: Upatanisho
Herbert Armstrong
alifundisha na kuwaelekeza watu wake kwamba sadaka zaweza kutolewa na
kuchukuliwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Upatanisho, wakati kwamba imekataza
sana kwa msisitizo mkubwa kufanya hivyo Kutoka 30:15, kodi ya Siku ya Upatanisho
ni changizo na hakuna mtu anayeruhusiwa kutoa zaidi au pungufu ya mwingine. Ni
amri ya Torati. Kodi hii ilikwisha tolewa kwa ajili yetu na Kristo (soma jarida
la Upatanisho
(Na. 138)).
Kwa ajili hii pia anakosa sifa za kustahili kuwa Eliya pia.
Mfano wa Jaribio wa 7: Maadhimisho ya Mganda wa Kutikiswa
Sadaka ya Mganda
wa Kutikiswa ni mkutaniko ulioamriwa wa Kanisa. Mambo ya Walawi 23:11 inaamuru
kutolewa kwa sadaka hii pamoja na makutaniko mengine yote (soma jarida la Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa (Na.
106b)). Herbert Armstrong hakuirudisha ibada
ya Sadaka hii ya Mganda wa Kutikiswa, na kwa ajili hii hana kigezo cha
kukubalika au kuaminika kuwa yeye ni Eliya.
Mfano wa Jaribio wa 8: Utakaso wa Hekalu Kwa Dhambi Zilizofanywa Kwa
Kupotoshwa au Bila Kukusudia
Biblia imeamuru kwamba
katika siku ya Saba ya mwezi wa Kwanza kufanyike mafungo ya saumu kwa kuzitubia
dhambi zilizofanywa pasi kukusudia na kwa kupotoshwa ili kujitakasa (Ezekieli
45:20; pia tazama jarida la Utakaso kwa Ajili ya
Dhambi za Kupotoshwa na Zisizo za Kukusudia (Na. 291)). Hii haikuwa ikifanyika kwenye huduma ya
Herbert Armstrong. Na kwa ajili hii hana kigezo cha kudhaniwa kuwa yeye ni Eliya.
Mfano wa Jaribio wa 9: Mwandamo wa Mwezi wa Kwanza
Utakaso wa Nyumba ya Bwana umetengwa maalumu katika siku hii (Ezekieli 45:18). Siku ya Kwanza ya Mwezi wa Kwanza ni siku ya kuitisha kusanyiko takatifu (Zaburi 81:3) (pia soma majarida ya Utakasa wa Hekalu la Mungu (Na. 241) na Mwezi-Mwandamo na Mwaka Mpya (Na. 213)). Hii haikuwa inaadhimishwa na kanisa la Worldwide Church of God wakati wowote ule. Haikuwa ikifundishwa au kutetewa na Herbert Armstrong. Kwa ajili hii pia hastahili kuchukuliwa kuwa yeye ni Eliya.
Mfano
wa Jaribio wa 10: Changizo kwa ajili ya Mfalme
Ezekieli 45:9-17 inaelezea wajibu wa changizo la falme (hii imeelezewa kwa kina kwenye jarida la Utoaji wa Zaka (Na. 161)). Hii haikuwa ikifanyika au kushughulikiwa wakati wa huduma ya Herbert Armstrong. Kwa ajili hii pia hawezi kuchukuliwa kuwa Eliya.
Mfano
wa Jaribio wa 11: Kipindi cha Pasaka
Kumbukumbu la Torati 16:6-7 inaelezea
kuhusu mchakato wa uadhimishaji wa Pasaka. Kanisa la Kwanza liliadhimisha kipindi hiki (soma
jarida la Pasaka (Na. 98)).
Kipindi cha Pasaka kinapaswa kuadhimishwa nje ya marago au majumba yetu. Katika
asubuhi ya Siku ya kwanza ya mapumziko na maadhimisho ya Idi ya Mkate Usio na
Chachu inaruhusiwa mtu kurudi nyumbani kwake. Herbert Armstrong hakufundisha
hivyo. Kwa ajili hiyo hawezi kuchukuliwa kuwa ni Eliya.
Mfano wa Jaribio wa 12: Unabii wa Uwongo
Maandiko
yanasema: Ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana
asubuhi. (Isaya 8:20). Herbert Armstrong akijua sana mambo hayo, bali
alifundisha kinyume chake na kinyume na Torati ya Mungu. Na pia alitoa nabii
nyingi na zisizohesabika za uwongo. (Soma jarida la Unabii wa Uwongo (Na. 269).) kwa ajili hii hawezi pia kuchukuliwa kuwa ni
Eliya.
Mfano wa Jaribio wa 13: Mioyo ya mababa na watoto wao
Eliya anakuja kuirejeza mioyo ya mababa kwa watoto wao na watoto kwa baba zao. Herbert Armstrong alishindwa kufanya hilo hata kwenye familia yake mwenyewe. Kwa ajili hii hawezi kustahili kuwa ni Eliya.
Mfano
wa Jaribio wa 14: Kurejesha Wimbo wa Musa
Jaribio au mtihani mwingine wa wateule ni kwamba wanauimba Wimbo wa Musa na Wimbo wa Mwanakondoo (Ufunuo 15:3). Wakati inapofanyiwa hoja ya kwamba huu Wimbo wa Mwanakondoo haujatolewa bado, ni upi basi kama sio ule Wimbo Uliobora (soma jarida la Wimbo Uliobora (Na. 145)), hakuna shaka kwamba Wimbo Uliobora umetolewa, na muziki wenyewe asilia unaweza au unapaswa urejeshwe – hii ilifanyika kwenye tukio la Usomaji wa Torati uliofanyika mwaka 1998 (soma jarida la Wimbo wa Musa Kwenye Kutoka 15 (Na. 179)). Herbert Armstrong hakufanya hivyo wala hakurejesha aina iwayo yote ya muziki au uimbaji wa kibiblia. Kwa ajili hii hawezi kustahili kudhaniwa kuwa yeye ni Eliya.
Hitimisho
Mtu hawezi kutuama kwenye shutuma za kiuvumi na kuendelea kulaumu kitu cha haki, mara nyingi kutoka kwenye kurasa za machapisho ya Kanisa lenyewe, kwa heshima isiyo na mashiko ya kuwaheshimu watu au kuwapendelea na akizivunja sheria za kibiblia na za kiraia. Kwa ajili hii tu peke yake inakithi matakwa. Ilivyo, kwa kweli, ni juu ya aibu isiyotiwa rangi kuona Kanisa likisamehe na kuvumilia maovu lililoyajua kuwa yalifanywa na Herbert Armstrong na huduma yake na sio tu kwa waumini waliobatizwa kwenye Kanisa bali pia kama watumishi waihudumuo Imani.
Hawakuwa ni watu 40,000 tu waliorudi majumbani, kama msomaji mmoja alivyosema kwenye ukurasa wa 4 wa jarida la The Journal: News of the Churches of God [Jarida: Habari za Makanisa ya Mungu]. Bali walikuwa ni mamia elfu kadhaa ya watu waliorudi nyuma, kwa kukata tama, na wengi wao walikuwa ni watumishi ambao kutokana na mambo yalivyokuwa walishindwa kuvumilia kwa yale waliyoayajua na kuyaona huko Pasadena.
Madai ya kwamba Herbert Armstrong alikuwa ni Eliya ni matusi kwa na kuchezea akili ya kila mtu mwenye busara na aliyesoma Biblia na kujaribu kutubu na kumfuata Kristo. Kanisa la Worldwide Church of God sio tu kwamba halikuyafanya marejesho ya vitu vyote wakati lilipolinganishwa na Kanisa linguine za zama zilizopita za kale – kama vile lile lililojulikana kama Seventh-Day Baptist Mill Yard Church la huko London, au la Wawaldensians wa Mashariki wa karne za kumi na tano na kumi na tisa – bali pia lilikosa ufahamu kwa kiasi kikubwa sana na lilikosa kuyajua utakatifu wa mafundisho na mafundisho makuu yaliyokaziwa kwenye zama za karne zilizopita.
Madaia ya kwamba Herbert Armstrong alikuwa ni Eliya ni jaribio dhaifu la kushambulia mambo ya msingi nay a muhimu. Jambo hilo ni agizo la kujaribu mambo yote, na kushika lile liliio la la kweli, na kuukazania wokovu aliyenao kila mti kwa hofu na kutetemeka. Mtu anayejificha nyuma ya madai kama haya, kwa kweli anasema: "Mimi nafurahia hali yangu ya ujinga na nitategemea juhudi za wengine ili kuniingiza kwenye Ufalme wa Mungu". Biblia inaonysha kuwa hilo haliwezekani. Sio wema wala ukarimu kwa mtu yeyote kuwaacha wao kwenye hali hii ya madanganyo ya kujidanganya mtu mwenyewe namna hiyo.
q